April 25, 2019



EMMANUEL Okwi anarejea kwenye ubora wake leo baada ya kufunga bao moja kati ya mabao 2-1 waliyoshinda leo mbele ya KMC uwanja wa CCM Kirumba.

Okwi alifunga bao hilo dakika ya 23 akimalizia pasi ya James Kotei na kuizamisha moja kwa moja kimiani, kipindi cha pili.

Hili inakuwa ni bao la tatu kwa Okwi akifunga mfululizo, alianza mbele ya Kagera Sugar akafunga pia mbele ya Alliance na leo mbele ya KMC na anafikisha jumla ya mabao 10.

 KMC walizidisha ushambulizi na kusawazisha dakika ya 57 lililopachikwa kiufundi na Hassan Kabunda akitumia makosa ya beki wa kupanda na kushuka Zana Coulibary.

Licha ya KMC kufanya mashambulizi mengi kupitia upande wa Zana bado walishindwa kupata bao la pili.

 Dakika ya 75 Simba walipopata penalti baada ya mchezaji wa KMC kuunawa ndani ya 18 penalti ambayo ilidakwa na Jonathan Nahimana kwa kumzidi ujanja Kagere ambaye staili yake ya kushtua iligunduliwa.

Dakika saba mbele Mzamiru Yassin akatengeneza penalti nyingine na mwamuzi wa mchezo, Kambuzi akaamua kutoa penalti kwa Simba iliyopigwa na nahodha John Bocco dakika ya 82.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 66 akijikita nafasi ya pili kwa idadi ya mabao ambayo anayo kibindoni tofauti na Azam FC.

Simba wamefunga jumla ya mabao 53 huku Azam FC wakiwa na mabao 49 kibindon kwa sasa.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Biashara United utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Karume.

3 COMMENTS:

  1. Kwanini wagome sasa hivi sio huko nyuma? Ingawa ni haki yao kuna kitu nyuma ya pazia.....Nyumba ya Yanga isafishwe....lakini pia sportspesa kama wadhamini si wanatoa pesa ya mishahara? Hapa kuna mkakati wa hujuma na kumtafuta ubaya kocha....ili aondolewe. Pia uchaguzi wa viongozi unatumika kama hujuma kwenye timu....usafi unatakiwa....kuondoa "magugu maji na takataka na mamluki"...Timu ya Wananchi na Wawekezaji ni Wananchi...Daima Mbele Nyuma Mwiko.....Yanga itashinda na itasimama imara siku zote!

    ReplyDelete
  2. Azam ashinde na kisingizio kiwe kwakuwa walikuwa hawajafanya mazoezi kutokana na migomo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic