MAURIZIO Sarri, Meneja wa Chelsea, leo atakuwa na kibarua cha kumenyana na kikosi cha Manchester United, amesema kuwa anahitaji muda wa misimu miwili kukibadilisha kikosi chake ili kufikia hatua ya kushindana na timu nyingine kubwa kutokana na adhabu ambayo wamepewa na Fifa ya kufungiwa kufanya usajili katika madirisha mawili ya usajili.
Licha ya vita inayoendelea kwa Chelsea kupambana kuwa ndani ya timu nne bora bado wana kumbukumbu ya kupoteza kwa peanalti mchezo wao wa fainali ya Kariobangi dhidi ya Manchester City.
Sarri amesema kuwa anapitia kwenye wakati mgumu kwa sasa ili kutimiza mipango ya klabu iliyopo ila atapambana kuona wachezaji wake wanacheza kwa kiwango bora na kama atapewa muda zaidi atafanikiwa.
"Nina uhakika katika hili, kama nitapewa misimu miwili nitakuwa nina uwezo wa kushindana na yeyote yule, ila sina uhakika katika misimu miwili hii kama tunaweza kuwa bora zaidi yao," amesema Sarri.








0 COMMENTS:
Post a Comment