April 26, 2019


  1. VITA ya mfungaji bora wa Ligi Kuu England inazidi kupamba moto kutokana na ushindani uliopo kwa wachezaji wa kila timu huku kila mmoja akionyesha juhudi ya pekee kuona namna gani anaisaidia timu yake kupata matokeo. 
  2. Mpaka sasa hakuna mbabe ambaye amejihakikishia namba moja kuwa yake jumla kutokana na idadi ya magoli kulingana kwa upande wa washambuliaji kwenye ligi hiyo.
  3. Washambuliaji watatu wote wametupia mabao 19 kinachowatenganisha ni idadi ya pasi za mabao walizotengeneza ili kumpata namba moja kwa sasa kama ifuatavyo:-
  4. Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Sergio Aguero mshambuliaji wa Manchester City ambaye ametupia mabao 19 akiwa ametoa pasi nane za mabao akifuatiwa na mfungaji bora msimu uliopita alitupia mabao 32 Mohamed Salah wa Liverpool ambaye ana mabao 19 na pasi saba za mabao.
  5. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Pierre Aubameyang anayekipiga Arsenal akiwa ametupia mabao 19 na pasi tano za mabao.
  6. Nafasi ya nne inashikiliwa na Sadio Mane wa Liverpool ambaye ametupia mabao 18 na ametoa pasi moja ya bao huku Raheem Sterling wa Manchester City akiwa nafasi ya tano na ametupia mabao 17 na ametoa pasi 10 za mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic