April 24, 2019


KUELEKEA kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Azam FC na Yanga utakaochezwa uwanja wa Taifa, Aprili 29, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amemtaja mchezaji tegemeo kwa kutupia mabao ndani ya Yanga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ten ameandika waraka huu:-

Yanga Africans Football Club, mabingwa mara 27 katika ligi kuu bara ,msimu wetu wa 2018/2019 tumecheza jumla ya mechi 32 tumeshinda mechi 23, tumetoka sare mechi 5 ,tumepoteza mechi 4 .

Tumefunga jumla ya magoli 51 na kufungwa jumla ya magoli 22 na kuweza kufanikisha jumla ya point 74.

Msimu huu tumecheza mechi 16 nyumbani,na kushinda mechi 14, tumetoka sare mechi 1, tumefungwa mechi 1 nyumbani, temefunga jumla ya magoli 34 na kufungwa magoli 13 pekee na kukusanya jumla ya point 43 kwa mechi za nyumbani.

Mechi za ugenini, tumecheza mechi 13, tumeshinda mechi 10, tumetoka sare mechi 1, tumepoteza mechi 3, tumefunga jumla ya magoli 27 na kufungwa jumla ya magoli 7 na kukusanya point 31.

Tarehe 29 .04.2019 tutakuwa na mechi dhidi ya Azam ,na tutakuwa mgeni wa Azam, tutarajie soka la anasa kutoka Yanga Africans, huku tukiongozwa na ncha yetu Kali ya kufunga magoli Heritier Makambo na yake style ya kushangilia ya ,"Make It Clap".

Kama kuipenda Yanga Africans ni dhambi basi moto haki yetu . ‘DAIMA MBELE NYUMA MWIKO’


4 COMMENTS:

  1. Ten bana
    Unataka kutuambia 16+12=32? na 10+3+1=13? You can't be serious. Sare na Simba, share na Ndanda, Share na Coastal Union bado ni sare moja ya ugenini? Hebu fanyeni mambo yenu kiuweledi bana msitu zingue. Yanga brand kubwa kufanya hivyo ni kudhalilisha brand yetu.

    ReplyDelete
  2. Popoyo at his best.Nawashangaa wanaomtilia maanani huyo mlugaluga .

    ReplyDelete
  3. Sometomes u need "Mchekeshaji ""

    ReplyDelete
  4. Yaani ni Vita kati ya Yanga vs TFF, Bodi ya Ligi, Waamuzi, Magazeti, Serikali....na maadui wengine.....sasa mechi ya Azam vs Yanga imehamishwa uwanja wa uhuru....YANGA NI IMARA....YANGA IMESIMAMA KIDETE YANGA INAJENGWA NA WANANCHI WASIOYUMBISHWA PAMOJA NA FITINA NA CHUKI LAKINI MWENYEZI MUNGU YUKO UPANDE WAO........"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic