April 27, 2019


KESI inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, juzi Alhamisi ilishindwa kuendelea baada ya mtuhumiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani kutokana na kuugua.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, Kelvin Mhina, juzi alipokea taarifa kutoka magereza mbele ya mahakama hiyo iliyosemaWambura alishindwa kufi ka mahakamani hapo kutokana na kuwa mgonjwa.

Hata hivyo, wakili wa upande wa serikali, Ester Martin uliiambia mahakama kuwa kwa upande wao serikali wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo kama kawaida.

Wambura anakabiliwa na mashitaka 17 likiwepo lile la utakatishaji wa fedha na kughushi nyaraka akiwa mfanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 9, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic