April 21, 2019


Klabu ya Yanga imeanza tena mazungumzo na Mlinda Mlango wa Bandari FC ya Kenya, Faruk Shikhalo ' De Gea' ili kumsajili mwisho wa msimu huu. 

Imeelezwa Faruk ambaye alikuwa golikipa bora wa ligi kuu ya Kenya msimu uliopita alipendekezwa na Zahera kusajiliwa katika dirisha dogo lililopita ila Yanga ilishindwa kumsajili kutokana na ukata.

Taarifa zinasema Yanga wana uhakika wa kupata saini ya kipa huyo kutokana na mkataba wake utakuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Hivi sasa Yanga ipo kwenye mikakati kabambe ya kuhakikisha inafanya usajili wa nguvu na kwa mujibu wa Kocha Zahera, hivi karibuni alisema usajili ujao utakuwa wa kufa mtu.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic