April 4, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewatahadharisha Shirikisho la Soka Tanzania kuwa makini na ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Zahera ameeleza kuwa iwapo TFF watakuwa makini na uendeshaji wa ratiba ya ligi ana uhakika wa Yanga kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amefunguka kwa kueleza kuwa timu yake ina uhakika wa kutwaa kikombe msimu huu endapo atashinda mechi zake 10 zilizobaki msimu huu.

Mbali na kushinda amewaombea Simba kupoteza walau mechi 3 kati ya 10 zilizosalia kwao ili kuwapa mwanya wa kukirejesha kikombe hicho baada ya kuchukuliwa na watani zao msimu uliopita.

Wakati huo kikosi cha Yanga leo kinashuka dimbani kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa ligi utakaopigwa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

4 COMMENTS:

  1. Maneno ya kupika siyo ya Zahera haya

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Zahera hajakata tamaa juu ya kufukuza na kukimbiwa na nyota wake baada ya msimu, lakini anaahidi kuwa atakijenga kikosi chake upya kwa mabilioni ya shilingi ambayo yanga watampa, anazidi kudai

    ReplyDelete
  3. kweli umekuwa bingwa sio wa TPL ni maneno

    ReplyDelete
  4. Simba chama langu fanyeni kweli Yanga huku "pumzi" imekata....gari la mkaa halifiki mwisho wa kituo...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic