April 21, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaka Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kutofuatilia mambo yasiyomhusu.

Kauli ya Zahera imekuja kufuatia Manara kumsema kocha huyo kuwa amekuwa akiishutumu bodi ya ligi na TFF kuwa inafanya mpango wa kuiwezesha Simba kuchukua ubingwa wa ligi.

Ameeleza kwa kumtaka Manara ni vema akafuatilia mambo yanayomhusu na kuachana na kumzunguzia yeye kwani anaona anachokifanya ni sahihi.

Zahera amesema kamwe hatoweza kukaa kimya kwani kila anachokisema ni sahihi kwake na hataweza kufumbia macho madudu ya TFF.

Amefunguka kwa kusema kama TFF wanaona anakiuka taratibu wamfungie lakini hatoacha kuzungumza mpaka pale uongozi wa Shirikisho hilo utakapobadilika.


2 COMMENTS:

  1. Manara atakuacha pale tu utakapoacha kuifuatilia simba kwani haikuhusu.

    ReplyDelete
  2. Haahaaa....chonde chonde Zahera usije kujishangaa uko Kalemie Congo na usijue umefikaje huko na kuiacha TFF ikiendelea na hamsini zake.Uliza mkongo man mwenzako marehemu Tambwe Leya akiwa kocha wa Yanga na Naby Camara wa Simba walivyofurumishwa kuondoka Taanzania.Wanakulia timing Papa Zahera.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic