April 21, 2019


UONGOZI wa Simba chini ya Bodi ya Wakurugenzi, umefanya kikao kujadili kama wamuongezee mkataba kocha wao mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems au wampotezee.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itoke kufungwa na TP Mazembe mabao 4-1 katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mkataba wa kocha huyo na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo Julai, mwaka jana alijiunga na timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano ni kwamba bado kuna hatihati kutokana na maazimio ya kikao cha bodi ya viongozi wa timu hiyo chini ya mwekezaji wake, bilionea, Mohammed Dewji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic