May 23, 2019

MSHAMBULIAJI wa timu ya Alliance FC, Dickson Ambundo amesema kuwa siri kubwa ya mafanikio ni kujituma na kufanya kile wanachoelekezwa na mwalimu wakiwa uwanjani.

Ambundo leo ametimiza vema majukumu yake kwa kufunga mabao mawili kati ya matatu ambayo yamewapa pointi tatu kwenye ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa uwanja wa Nyamagana.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ambundo amesema kuwa ushirikiano wa timu pamoja na maelekezo ya mwalimu yanawasaidia kupata matokeo chanya.

"Tunajua kwamba tukiwa uwanjani tunahitaji pointi tatu hivyo tunashirikiana na kufuata maelekezo ya mwalimu kwa ajili ya kutimiza majukumu yetu, mashabiki pia sapoti yao ni kubwa," amesema Ambudo.

Ushindi huo unaifanya Alliance kuwa na uhakika wa kubaki ligi kuu msimu ujao baada ya kucheza michezo 37 na imejikusanyia jumla ya pointi 47 ikiwa nafasi ya tisa na ina mchezo mmoja mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic