May 3, 2019


USHINDI wa mabao 3-1 walioupata jana mbele ya Valencia Uwanja wa Emirates ikiwa ni mchezo wa nusu fainali Ligi ya Europa umemfurahisha Meneja wa Arsenal, Unai Emery na kusema kuwa hicho ndicho walichokihitaji sasa kazi kubwa itakuwa mchezo wao wa marudio wakiwa ugenini.
"Tulihitaji kushinda na hicho ndicho tumekipata haikuwa rahisi kwetu kupata matokeo kwani mambo yalikuwa magumu pia upande wetu, bao letu la mwisho limekuwa bora sana kwetu licha ya kutoshana nguvu kwa upande wa umiliki wa mpira na mbinu.
Mshambuliaji Pierre Aubameyang amesema kuwa vipigo vitatu mfululizo walivyovipata vimewapa hasira ya kupambana na wanaona fahari kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Valencia.
Aubameyang alimaliza kwa kufunga bao la mwisho dk ya 90 kwa Valencia baada ya Laccazette kuanza kusawazisha bao lililofungwa dakika ya 11 na Diakhaby kwa  kuanza kucheka na nyavu dk ya 18 na 25.
Alexandre Lacazette amesema kuwa mchezo wao wa marudio utakuwa na ushindani mkubwa kwani alipata nafasi mbili za kufunga mabao na akafanikiwa kufunga.
"Nafasi mbili nilizozipata nimezitumia, pia nampa pongezi, Aubameyang kwa kupachika bao la tatu limetuongezea mtaji na nguvu ya kupambana," amesema Lacazette. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic