May 7, 2019


BAADA ya jana kubeba pointi tatu kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui uwanja wa Uhuru, sasa hesabu zao ni kuelekea mchezo wao wa Mei 9 dhidi ya Azam FC utakaochezwa uwanja wa Chamazi.

Azam mchezo wao wa mwisho wa ligi walilazimisha sare mbele ya Stand United kwa kufungana bao 1-1 hivyo itakuwa ni muda wao kutumia vema uwanja wa nyumbani kupata pointi tatu.

Mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Uhuru walitoka sare ya kufungana mabao 2-2 hivyo mchezo wao ujao utakuwa ni wa kulipizana kisasi.

KMC imecheza michezo 34 ikiwa nafasi ya sita na pointi 45 huku Azam FC wakiwa wamecheza michezo 34 wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 67.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic