May 3, 2019



Kocha Mkuu wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa wapo 'siriazi' na ligi hivyo watapambana kutoshuka daraja.

Ushindi wao mbele ya Lipuli kwa mabao 3-0  umeipandisha Biashara kutoka nafasi ya 19 mpaka nafasi ya 16 baada ya kufikisha jumla ya pointi 37 na wamebakiwa na michezo mitano.

Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa ana imani na ubora wa kikosi chake kutokana na nia waliyonayo kubaki kwenye ligi msimu ujao.

"Hatuna utani kwa sasa, tunajua tumebakiwa na mechi chache ila kwetu zina maana, nimewaambia wachezaji wangu hakuna dawa itakayotubakiza kwenye ligi zaidi ya kushinda mechi zetu.

"Hivyo kwa kuanza tumeanza na Lipuli kisha wengine wanaofuata watajua kwamba tunamaanisha kile tunachokisema tutapambana ili kubaki msimu ujao," amesema Said.

1 COMMENTS:

  1. Big up team Biashara, hakuna kukata tamaa hadi dk ya mwisho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic