May 3, 2019


UONGOZI wa JKT Queens umesema kuwa hawatapoteza hata mechi moja mpaka mwisho wa msimu kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania inayodhaminiwa na bia ya Serengeti ili kuweka heshima kwa wapinzani wao.

Kocha Mkuu wa JKT Queens, Ally Ally amesema kuwa wengi wanadhani timu yake ni ya kubahatisha ilihali imetwaa ubingwa hivyo ili kulinda heshima ni lazima washinde mechi zote.

"Tumepambana na kufikia lengo letu la kutwaa ubingwa kama ambavyo tulikuwa tunahitaji, sasa kazi iliyobaki ni kuendeleza rekodi ya kutofungwa mpaka msimu huu.

"Michezo yetu minne ambayo ipo mikononi mwetu haitupi presha tutapambana kupata ili tushinde mechi zetu kama ambavyo tulianza ndivyo ambavyo tutamaliza,"

JKT Queens wamecheza mechi 18 na kushinda zote na kujikusanyia pointi 54 kama watashinda mechi nne zilizobaki watamaliza wakiwa na pointi 66.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic