May 4, 2019


NDEGE aina ya Boeing 737 imeshindwa kutua na kuishia kuingia mtoni nchini Marekani.

Hiyo ni aina ileile ya ndege iliyopata ajali na kusababisha vifo vya mamia ya watu nchini Ethiopia na Indonesia.

Kwa mujibu wa habari, ndege hiyo ilitoka katika barabara yake na kuingia mtoni wakati ikitaka kutua Florida nchini Marekani.

Tukio hilo limetokea katika uwanja wa ndege wa Jacksonville,ambapo ndege hiyo ya abiria iliyokuwa imebeba abiria 136 na wafanyakazi wa ndege hiyo ilishindwa kutua na mwisho kuingia katika mto wa St.John.

Hata hivyo hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha isipokuwa watu wawili wamejeruhiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic