May 4, 2019


KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kikosi chake kipo fiti kuivaa Lipuli ya Seleman Matola anaamini atashinda mchezo wake wa Jumatatu ikiwa ni hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho.

Zahera amesema kuwa anatambua kwamba Lipuli ni wazuri wakiwa nyumbani licha ya kuwafunga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uwanja wa Samora wasitarajie watafanikiwa tena.

"Sikuepo wakati timu ya Lipuli inaifunga Yanga, ila nilikuja kuangalia ripoti na matokeo nikagundua kwamba, wapinzani wetu walibahatisha kwani walipiga shuti moja kwenye lango na wakatufunga bao moja.

"Sasa nikawaambia vijana wangu mmecheza vizuri, msiwe na mashaka huu ni mpira tukikutana nao wakati mwingine lazima tushinde, hivyo tutaingia kwa mbinu mpya kutafuta matokeo," amesema Zahera.

Mshindi wa mchezo wa jumatatu, atakutana na Azam FC  ambao walishinda jana kwa bao 1-0 mbele ya KMC.

6 COMMENTS:

  1. Haya Zuhura!hawachezi kwa maneno!

    ReplyDelete
  2. Acha dharau hizo huyo anaitwa Zahera na ww nahisi akili hauna kwamba haujui kazi ya Zahera au et azam 5 yanga 1 ikaja azam 0 yanga 1 hakuna kama Zahera timu no hela point 80

    ReplyDelete
  3. Yule refa aliyechezesha mechi ya Azam vs Yanga anapaswa kufungiwa!aliwabeba Yanga hadi inatia kinyaa.Goli la Ngoma lilikataliwa...halali na wala hakuwa amenawa.Pia alifanyiwa faulo na Kindoki ambayo ilistahili penalty.Kupendelewa apendelewe Yanga...Ikiwa Simba hata ambako haijapendelea Zuhura anamaka!Azam bado itakula sahani moja na Yanga, kwa mchezo ule wa kupaki basi Zuhura atapata tabu sana

    ReplyDelete
  4. hana akili kabisa Zuhura!

    ReplyDelete
  5. zuhura alikuwa amekuja kuisaidia wakati timu yake inaadhibiwa na lipuli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic