May 29, 2019


Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imetangaza kufanya marekebisho katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku ikisema itachukua hatua kwa watunza takwimu wake waliopotosha.

Awali ilionekana Kagera Sugar ndio imeteremka lakini Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema marekebisho waliyofanya Stand United inashuka na nafasi ya juu inakwenda kwa Kagera Sugar.

Maaana yake Stand United ndio iliyoteremka daraja na nafasi ya kucheza Play Off inakwenda kwa Kagera Sugar.

Kagera Sugar itaivaa Pamba Juni 2 katika mechi ya Play Off na mshindi atacheza Ligi Kuu Bara na Mwadui FC itamenyana na Geita.

Baada ya ligi kumalizika jana, kumekuwa na gumzo na kizumgumkuti huku watu wakiwa hawajui timu iliyoteremka kwa kuwa tawimu za Gazeti la Championi na Azam Tv zilionyesha aliyeshuka ni Stand United huku takwimu za bodi ya ligi zilionyesha ni Kagera Sugar ndio iliyoteremka.

2 COMMENTS:

  1. Kwa ufupi mmeboronga kila pahala wal sio hapo tu wala hamjui mtendalo mpo mpo tu kwa kweli nyinyi ni mzigo mzito uliomshinda hata Mnyamwezi

    ReplyDelete
  2. Hahahahaaaaaaa...hii ni ligi yenye maajabu duniani..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic