May 24, 2019

KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa haikuwa rahisi kupata ushindi mbele ya Tanzania Prisons kutokana na kila timu kumkamia mwenzake ili kupata pointi tatu.

Jana Castal Union waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Raizin Hafidh dakika ya 70 uwanja wa Mkwakwani na kuifanya timu hiyo kuwa na uhakika wa kubaki kwenye ligi msimu ujao.

Mgunda amesema kuwa kwa namna ligi ilivyo kwa sasa timu nyingi zimepishana kwa pointi chache hivyo kila timu inapokutana na mpinzani inacheza kwa kukamia zaidi ya fainali.

"Kwa sasa ligi inazidi kuwa ngumu licha ya kwamba ni lala salama, kila timu inayoingia uwanjani inacheza kwa kukamia ili kupata pointi tatu, ila nnafurahi kwa kuwa tumeshinda bado tunaednelea na mapambano," amesema Mgunda.

Coastal Union imefikisha jumla ya pointi 47 baada ya kucheza michezo 37 ipo nafasi 10 kwenye msimamo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic