May 24, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Adam Salamba amesema kuwa kitendo chake cha kuomba viatu kwa mchezaji wa Sevilla jana hakikuwa na lengo baya bali ni 'Fair Play' kwani viatu anavyo vya kutosha.

Kwenye mchezo wa Jana uliochezwa uwanja wa Taifa na Simba kukubali kupoteza kwa mabao 5-4, Salamba alionekana akionyesha ishara ya kuomba viatu kwa mchezaji wa Sevilla.

"Haikuwa kwa ubaya mimi kufanya vile bali ni fair play, nadhani nimewakosea mashabiki na viongozi wangu wa Simba napenda kuwaomba radhi, kwani kama viatu ninavyo vya kutosha na vyenye ubora," amesema Salamba. 

Sevilla waliletwa kwa hisani ya SportPesa na walitembelea vivutio mbalimbali nchini Tanzania.

3 COMMENTS:

  1. Viatu ni sehemu ya jezi. Salamba hukutakiwa kuomba radhi kwa sababu ni sawa na anayeomba shati la mchezaji mwenza. Ni kawaida sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic