May 4, 2019

IMEELEZWA kuwa sababu kubwa iliyomfanya mgombea wa nafasi ya ngazi ya Uenyekiti katika uchaguzi Mkuu wa timu ya Yanga, Mbaraka Ingangula kujiengua ni ufunjifu wa katiba na utaratibu uliowekwa kwa ajili ya uchaguzi na vitendo vya rushwa.

Yanga kesho wanatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi ambao watadumu miaka minne kwa ngazi tatu ambazo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Igangula amesema kuwa aliamini atashinda nafasi hiyo ila ameona bora aachie ngazi kwani yeye ni muumini mzuri wa kufuata katiba ya klabu pamoja na ile ya nchi.

"Nikiwa ni muumini mzuri wa kufuata na kuheshimu katiba yetu ya Yanga na nchi kiujumla siwezi kuwa msaliti kwa kuzisigina katiba hizo, na pia siwezi kuthubutu kwenda kinyume na msimamo wa Rais wetu John Magufuli, kuna ukiukwaji mkubwa na uvunjivu wa katiba hivyo ni bora nijiweke pembeni.

"Kwa hali ya uvunjivu wa katiba pamoja na masuala ya rushwa ninaamua kujitoa kwenye kiny'anganyiro cha uchaguzi unaoendeshwa kinyume na katiba na hii ni kulinda na kuiheshimu katiba yetu," amesema Igangula.

3 COMMENTS:

  1. Hana lolote ashausoma upepo.bora umejitoa mwenyewe maana kesho ungeaibika bure. Tewndeni na Msolla na Mwakalebela!

    ReplyDelete
  2. Wakati anachukua form hakuona hilo!? Kwahiyo yeye ndo alituma watu mahakamani ili waendelee kupiga dili!? After all amewahi kuwa kiongozi yanga, hakuna jipya

    ReplyDelete
  3. Watani fanyeni uchaguzi kistaarabu na msifanye fujo.kila la kheyr katika uchaguzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic