May 4, 2019


KIUNGO Mkabaji wa timu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambaye ni kipenzi cha mashabiki, Jonas Mkude amesema kuwa Taifa limepata pigo kwa kuondokewa na Dk.Reginald Mengi.
Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP alifariki Usiku wa kuamkia Juzi ikiwa ni miezi sita imepita tangu kufariki kwa aliyekuwa mkewe, Mercy Mengi akiwa Dubai, kwenye Falme za Kiarabu alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mkude amesema kuwa mengi aliyoyafanya Mengi ni funzo kwetu binadamu ambao bado tunaishi kwa mapenzi ya Mungu hivyo ni lazima tutambue kwamba njia yetu ni moja.
"Ameacha pengo kwani alikuwa ni mtu wa kujitoa, ila hatupaswi kulaumu zaidi ya kushukuru na kumuomba Mungu, njia yetu ni moja hatuwezi kukwepa hilo, inauma ila tunapaswa tumuombee kwa Mungu ampunguzie  adhabu za kaburi ," alisema Mkude.
Dk.Mengi pia alikuwa ni mtu wa michezo kwani alikuwa mshauri wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na kuwa ndani ya kamati ya maandalizi ya timu ya Taifa ya Vijana ,Serengeti Boys akiwa ni mlezi. 

Kwa mujibu wa msemaji wa familia Michael Ngalo amesema kuwa mwili wa Mengi utapumzishwa kwenye makazi yake ya milele siku ya Alhamisi, kijijini kwake, Nkuu, Machame.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic