May 4, 2019



KAKA wa mchezaji wa Manchester United, Florentin Pogba amesema kuwa ni suala la kusubiri wakati kwa mdogo wake kujua kama ataondoka ndani ya Manchester United kwenda Real Madrid ambapo amekuwa akihusishwa kwenda.

Mpaka sasa Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameshindwa kuelewa kama Pogba mwenye miaka 26 atabaki kwenye kikosi chake msimu ujao.

"Kwenye mpira jambo lolote linaweza kutokea, ila kwa sasa sijui nini kinaendelea kwa Pogba na Manchester United.

"Leo ninaweza kukwambia jambo hili na kesho kikatokea kitu kingine, haya yote yatakuwa wazi baada ya muda kupita, tusubiri na tuone kama ataondoka ama atabaki," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic