May 4, 2019


LICHA ya ushindi walioupata juzi, uwanja wa Uhuru mbele ya Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemvaa bki wake wa kushoto Paul Godfery pamoja na wachezaji wenzake kwa kucheza chini ya kiwango.
Yanga ilishinda mabao 2-1 kwenye mchezo wao wa ligi na kuifanya ijikite kileleni ikiwa na jumla ya pointi 80 baada ya kucheza michezo 34, mabao ambayo yalifungwa na Pappy Tshishimbi aliyemalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na Heritier Makambo aliyemalizia pasi ya Paul Godfrey.
Zahera amesema alishangwaza na mchezo waliocheza wachezaji wake wakiongozwa na beki, Paul Godfrey ambaye alitoa pasi ya mwisho ya ushindi kwa Makambo.
"Kabla ya mchezo niliwaambia wachezaji wangu wanapaswa kufunguka upande wa pembeni ambao alikuwa anacheza huyu Paul, sasa yeye akawa anajichanganya na wenzake anafuata mipira kati majukumu ambayo hayakuwa yake.
"Tulipata taabu kushinda bao la pili kwani tuliruhusu kwenda mapumziko tukiwa tumetoshana nguvu, haikuwa mpango wangu kucheza vile, niliwaambia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kama tutaendelea kufanya hivyo hatutapata ushindi, ndio maana walipofunguka tukapata bao la pili la ushindi," amesema Zahera.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic