May 19, 2019


MABINGWA watetezi Simba leo wamebeba pointi tatu mbele ya Ndanda FC na kuanza kunukia ubingwa wa ligi msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Meddie Kagere kipindi cha kwanza amepachika mabao yote mawili ambapo bao la kwanza amefunga dakika ya tatu akimalizia pasi ya John Bocco na bao lake la pili alifunga dakika ya 11 akimalizia pasi ya Clatous Chama.

Ushindi huo umewapa nafasi Simba kujikita kileleni wakiwa na jumla ya pointi 88 na wamebakiwa na michezo mitatu ili kukamilisha mzunguko wa pili.

Kwa nafasi ambayo kwa sasa Simba wamefikia wanahitaji pointi mbili ili kujihakikishia kutetea ubingwa wao msimu huu.

Simba wamepiga jumla ya mashuti 10 ambayo hayakulenga lango huku Ndanda wakipiga jumla ya mashuti sita ambayo hayakulenga lango.

Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Singida United utakaochezwa uwanja wa Namfua Mei 21.

7 COMMENTS:

  1. Sio kunukia lakini wapigs hodi

    ReplyDelete
  2. Point mbili nini..ni moja tu kwana hata alilingana point na Yanga simba bado inaizidi Yanga zaidi ya magoli ya kufunga zaidi ya ishirini..Hivyo akitoa sare moja na mechi nyingine mbili hata akifungwa Simba bado atakuwa bingwa

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Naona kama tayari wameshachukua ubingwa. Yanga ashinde mechi zake 2 zilizobakia , Simba atoe sare moja tu aparte pointi moja tu kati ya mechi zake 3 zilizobakia, wote Yanga na Simba watafikisha pointi 89. Sasa kwenye magoli ndio balaa. Itabidi Yanga ashinde katika game zake na Azam na Mbeya City, magoli 30 na zaidi. Haitokeagi hilo. Hivi Simba katika game 3 hawezi kupata pointi moja ? Nido maana nasema Simba tayari Bingwa.

    ReplyDelete

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsantee kwa kulitambua hilo kuwa simba Bingwa

      Delete
    2. HILI LIMEKWISHA HALINA UBISHI SASA NI WAZI KABISA

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic