FT: Mbeya City 1-2 Simba
Uwanja: Sokoine
Kipindi cha pili dakika 90 zimekamilika zinaongezwa dk 4
Meddie Kagere Goooal dk ya 84
Jonas Mkude Goooal Simba dakika ya 67
Okwi anaingia ndani Mo Ibrahim anakwenda benchi kipindi cha pili.
Mpira kwa sasa ni kipindi cha pili
Kipindi cha kwanza, zinaongezwa dakika tatu
Goooooal Iddy Nado dk ya 22
Nyoni anaingia kuchukua nafasi ya Paul Bukaba ambaye ameumia dk ya 30.
MBEYA City leo wameikaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Sokoine muda.
Kipindi cha kwanza, Iddy Nado anaitanguliza Mbeya City kifua mbele kwa kufunga bonge moja la bao akiwa nje ya 18 baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe na kumsindikiza kwa macho.
Saa moja kabla ya mchezo wa leo, mvua ilinyesha ila kwa sasa imekata na mpira unaendelea bila wasi.
Mashabiki wamejitokeza kwa wingi uwanja wa Sokoine kushuhudia kandanda safi la kukata na shoka.
anaongoza simba au mbona sielewi
ReplyDeleteUmeandika Simba 1 Wakati Mbeya City Ndo Wana Gaol 1 Kuwa Makin Bwana Ktk Uandishi
ReplyDeleteSimba wabadilishe kocha huyu siye kocha. Kila mchezaji anacheza mwenyewewe tu. Sio mpira wa kufundishwa. Ni aibu kwa Mo dewji kutumiya billions ya shillingi huku unafungwa na timu ya millioni moja.
ReplyDeleteAcha kupanic Subiri mpira uishe ndio ucomment
DeleteWe hujui mpira kabisa, tumefika robofainali na kocha huyu makocha wangapi wameifikisha robofainali simba.
DeleteKuna watu wengine ni mashabiki wa ngoma za jadi halafu wanajifanya wana utaalam wa soka.Sometimes uchezaji wa timu ki ujumla unategemea na aina ya timu unayokutana nayo na mazingira ya uwanja.
DeleteKstika mchezo WA leo aliitumia Kocha WA Simba Kama vile kuwajaribu wachezaji badala ya kutafuta pointing tatu muhimu na aendelee na siasa hiyo michezo ijayo
ReplyDeleteMechi zimeongozana anajaribu kurotate wachezaji, anahofia kuchoka wachezaji siku moja wanapumzika. Tuiombe simba kila game ishinde
Delete