May 3, 2019

KOHA Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kuwa hawajafungwa na Simba bali wamefungwa na waamuzi wa mchezo ambao wameshindwa kutimiza sheria 17.

Mbeya City wamepoteza mchezo wa leo kwa kufungwa mabao 2-1 licha ya kuanza kutangulia kufunga kipindi cha kwanza kupitia kwa Iddy Nado ambaye alitumia makosa ya mabeki wa Simba waliokuwa wakikaba kwa macho.

Nsanzurwimo amesema kuwa hajajua sababu ya faulo ya pili ambayo Simba wamepewa licha ya kuutazama mchezo kwa umakini hali iliyofanya wapoteza mchezo wao.

"Hii ni kazi ya mtu, sasa kama inatokea mtu mwingine anaiharibu kwa makusudi hii sio sawa, ilikuwa ni lazima tushinde na tulipambana kweli matokeo yake Simba inashinda mabao 2-1 siamini kama nimefungwa na Simba bali nimefungwa na waamuzi.

"Najua Simba ni timu kubwa ila haipaswi kupewa kipaumbele kila mara hata kama inakosea, ukitazama mabao yao na namna ambavyo wamefunga sina namna ya kukubali na kuwaomba waamuzi wawe makini wakati mwingine, vijana wangu wamechoka kwa kupambana kisha haki yao inapotea," amesema.

Mabao ya Simba ya leo yote mawili yalifungwa kwa kutengenezwa na adhabu ambapo lile la kwanza lilifungwa na Jonas Mkude baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na la pili lilifungwa na Meddie Kagere baada ya Hassan Dilunga kuchezewa faulo. 

17 COMMENTS:

  1. Marefa wako sawa usitafute sababu

    ReplyDelete
  2. Sasa hivi imeshakua ni kamtindo kila anaefungwa na simba anasingizia Refa. Sote tumeona mchezo ulikua fair kabisa.juzi mlisema uliongezwa dakika 7 ili simba akomboe,leo tumeona simba anaongoza na bado dakika 5 ziliongezwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mfa maji lazma atape tape waacheni na mateso yao

      Delete
  3. Sasa wewe ulitaka faulo zipuuzwe ili Simba ifungwe? huyo Kocha inafaa apeane mikono na Zahera

    ReplyDelete
  4. Kocha bonge la kauzu huyu mimi simwelewi hata chembe ya malalamiko yake!

    ReplyDelete
  5. mbonaa hasemi ile penati ya Okwi kwanza yuko kwenye nafasi gani ya msimamo hadi adai timu yake inaonewa

    ReplyDelete
  6. Imekuwa fasheni ukicheza na Simba useme umeonewa ili kuficha udhaifu wako.Kila mjinga anayefungwa ameonewa.

    ReplyDelete
  7. huyo kocha kanda moja na wa Yanga.Wanalalamika bila sababu za msingi.Sasa ina maana wachezaji wa Simba wakifanyiwa madhambi basi marefarii wapete au basi mechi za Simba waruhusu wapinzani wachague marefarii wanaowataka.Wakiifungwa Simba,aah refarii wamecheza kwa haki ila akishinda Simba, mmh refarii kawebeba.Mashabiki na makocha kuweni fair na ninawashauri kufuatilia kipindi cha kipenga chetu kinachoonyeshwa na AZAM TV na kinachoendeshwa na marefarii wastaafu kina Othman Kazi ambao wanachambua kwa mwongozo wa sheria 17 za mpira wa miguu.
    Nawashauri makocha wawe wanafuatilia marejesho ya mechi zao na wanipe takwimu za Simba ambazo wamecheza nao na zinaonyesha possesion ya mechi za Simba kama Simba waliwahi kumiliki chini ya asilimia 50.Na kwa utathimini wa kocha anayejua maana ya soka basi ataelewa ni kwa nini Simba wanapata advantage ya faulo nyingi kuliko timu wanazokabiliana nazo.Refarii ana sababu ya kutoa adhabu inayostahili na sio ili mradi kupeta tu.Muhimu ni marefarii ni kujiamini na kazi yao na kutia pamba masikioni.

    ReplyDelete
  8. Watanzania watu wa ajabu sana.. kitu kipo wazi.. ila ni kupanua midomo tuu.
    Kocha wa Simba alipanga kikosi mwanzoni ili asome mchezo... mbeya city walivokaza.. naye kapiga sub zenye akili.. kakaza mara mbili.. kipindi cha pili mmeona mb.city walivyokimbizwa hadi wakadhani mchezo umekuwa 120 min.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MPIRA WOTE TUMEONA SIMBA KAPAMBANA KUPATA USHINDI ALIKUWA NYUMA KWA GOLI MOJA MPAKA DAKIKA 45 ZA KWANZA ZINAISHA, LEO WAMERUDISHA GOLI NA KUFUNGA LA KUONGOZA, MTU ANAROPOKA ANASEMA REFA KAPENDELEA SIMBA, TENA KOCHA, BASI ANA MATATIZO TUMUHURUMIE TUU MAANA ATATESEKA SANA MPAKA LIGI IISHE.

      Delete
  9. Marefa wanakazi sana,wanalaumiwa kila siku

    ReplyDelete
  10. Eti refa kashindwa kutafsiri sheria 17 za mpira. Hivi labda kwa uelewa wang mdogo naomba kuuliza, hivi sheria zote zinamhusu refa. Kuna sheria inahusu uwanja uweje, wachezaji wawe wangapi, muda wa mchezo n.k sasa refa tena si ajabu wa kimataifa mbele za watu eti refa hakuzingatia sheria 17 duuhh! Hebu ninyamaze mie sio familia ya mpira.

    ReplyDelete
  11. Oyaa nyie timu mbeleko mkishtukiwa muwe mnanyamaza basi, yaan kila timu inawalalamikia ninyi tu? Kikisi One billion ushindi hadi kwa mbinde? Halafu msiambiwe loh

    ReplyDelete
  12. Wewe timu Omba Omba mmeshindwa uwanjani mmeanza kampeni uchafu nazo zitashindwa.Kachezeni nyie sasa umebaki zamu yenu.Tumefunga magoli mengi kuliko timu yeyote nä tumefungwa magoli machache kuliko timu yeyote kwenye ligi.Tunafukuza mwizi nä sasa ameanza kuweweseka.Bado mechi 6 ubingwa urudi nyumbani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic