May 1, 2019


MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kitapata taabu sana kupambana na kikosi cha Barcelona leo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali utakaochezwa uwanja wa Nou Camp.
Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England  itamenyana na Barcelona inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ambao kwa sasa ni mabingwa wapya wa La Liga, majira saa 4:00 Usiku.
Klopp ambaye aliiongoza Liverpool kwenye fainali ya mabingwa mwaka 2018 mbele ya Real Madrid amesema: 
"Tulikuwa kwenye mashindano haya mwaka uliopita na tulifika hatua ya fainali, lakini utakuwa mchezo mgumu kwetu na ninajua nitapata taabu kwenye mchezo huo ila nina nafasi ya kupata matokeo.
"Uzoefu nilionao pamoja na mafanikio ambayo tuliyafikia mwaka uliopita unatupa matumaini ya kupata matokeo kwenye mchezo wetu ambao una presha kubwa kwa kila mmoja," amesema Klopp.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic