May 4, 2019


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hajaridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa kati hali iliyowafanya wakapoteza mchezo wao wa jana mbele ya Singida United.


Mtibwa Sugar ilipoteza mchezo wake huo uliochezwa uwanja wa Namfua kwa kufungwa mabao 2-1.

Katwila amesema kuwa ingekuwa ni maamuzi yake mwamuzi huyo wa kati angemfungia ila yeye hana uwezo huo anawaachia wenye mamlaka ambao ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Sio maamuzi mazuri, huyu mwamuzi ni mara ya pili kutuchezesha na bado anashindwa kumudu mchezo hivyo anatuvuruga na tunashinwa kuelewa anachokifanya, naiomba mamlaka husika iweze kuchukua hatua.

"Mpira ni fair, kwa kuwa anafanya maamuzi ambayo si sahihi, kama ametufanyia mbele ya Singida kuna siku Singida nao watasafiri watakutana na watu wenye tabia hizi hii sio sawa," amesema Katwila.

Ushindi huo unaifanya Singida United kutinga kwenye 10 bora wakiwa wamecheza jumla ya michezo 34 nafasi ya sita na wana pointi 43.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic