May 17, 2019

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kesho wataanza mazoezi kwa ajili ya kuiwinda Ndanda mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Simba, Abas Suleiman amesema kuwa baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar, wachezaji wote walirejea nyumbani hivyo kesho watarejea kambini.

"Baada ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar wachezaji walirejea majumbani kwao, hivyo kesho watarejea kambini na kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ndanda.

"Maandalizi yapo sawa na tuna imani ya kupata matokeo chanya hasa kutokana na umuhimu wa mchezo wenyewe, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Suleiman.

1 COMMENTS:

  1. Kumbuka Ndanda ndio waliokuwa wa mwanzo msimu huu wa ligi kuisimamisha Simba kwa hivyo ukosefu makini wa aina yeyote kwa Simba dhidi ya ndanda kunaweza kuiacha msimbazi kimya na wasiamini kuona kinachotokea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic