May 17, 2019


KUELEKEA kipindi cha usajili, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amefunguka kuwa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu atabaki Yanga, suala la kuondoka ni uamuzi wake.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa za nyota huyo kusaini mkataba wa awali Simba kwa ajili ya msimu ujao.

Ajibu alijiunga na Yanga msimu wa 2017/18 akitokea Simba ambapo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Msolla alisema kuwa lengo lao ni kumbakisha Ajibu pamoja na wale wachezaji ambao benchi la ufundi litahitaji kufanya nao kazi kwa msimu ujao.

Msolla alisema kipindi cha usajili kikiļ¬ ka kocha ndiye mwenye maamuzi ya mwisho wa kuamua ni mchezaji gani ambaye atabaki katika kikosi hicho.

“Ajibu ni mchezaji wetu na malengo ni kuendelea kubaki hapa Yanga ndiyo maana tunatafuta fedha kwa bidii kuona wachezaji wetu wanakuwa imara msimu ujao ingawa ni uamuzi wake kuondoka na lazima ajipime na kujitafakari mwenyewe.

“Tunapambana kuona msimu ujao tunakuwa na wachezaji ambao watakuwa imara na kutengeneza timu yenye ushindani katika ligi pamoja na kimataifa ndiyo maana tutamsikiliza mwalimu,” alisema.

Ajibu mpaka sasa msimu huu amefanikiwa kufanga mabao sita huku akitoa asisti 17 katika mabao 55 ambayo yamefungwa na kikosi hicho kwenye mechi 36 na wakiruhusu mabao 25.

5 COMMENTS:

  1. Anasema tunatafuta pesa Kwa bidii ina mana mpaka sasa bado hakunan

    ReplyDelete
  2. Wanayanga wavunjika moyo....kuna kirusi kimeingia

    ReplyDelete
  3. Mimi nilifikiri kuwa Uongozi Mpya umeingia mambo yanaenda kuwa na "afueni" pale Yanga imekuwa tofauti....kwani wachezaji tegemeo wanauzwa....mechi za zikiendelea, sherehe za Michango zinasitishwa na kuahirishwa, Kocha anakimbia/kwenda nje kuuza mchezaji, ahadi hewa na michakato na uongo kila kukicha....sasa sijui wana nia ipi? Wanayanga hebu jibuni haya maswali kabla chombo "akijaenda mrama"....msipumbazwe, Simba wanafurahia hii hali yenu.....kumekuwa na jitihada za kuwapotosha na kuwahadaa na kuwaridhisha wakati chombo hakiendi sawa.....msilale Yanga amkeni....."wanawapetipeti" kwa lugha za kuwalainisha mitandaoni....lakini ukweli ni kuwa hawana nia ya kuona Yanga inaimarika.....Fanyeni uchunguzi kwani kila maoni ya kupata wachezaji bora, benchi bora la ufundi na mambo mengine ya kuimarisha timu yanapotolewa utaona wanasema msajilini mchezaji fulani (wa bei ya chini kutoka hapa Tanzania tena mwenye kiwango cha kawaida, na ambae anatoka Simba au hata timu nyingine hali kiwango chake hata Simba hafai) ....Yanga kama mnataka maendeleo msikubali kuyumbishwa takeni na himizeni yaliyo juu hasa nikimaanisha usajili wa wachezaji level juu). Pili suala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji lazima wawekezaji waanze kutafutwa ndani ya miezi 3....
    Kuna upotoshwaji na nia ya kutaka kuwatoa Yanga "nje ya reli/mstari"....wanachama na mashabiki amkeni sasa hivi mkihoji hivi vitu kabla vitu havijaharibika.....Uongozi huu lazima hukidhi matakwa ya wanayanga kuwa na timu bora....lakini dalili ya mvua ni mawingu.....nina maana kila mtu alifikiri Yanga itafanya usajili bora na kuanza kusuka kikosi bora haraka, lakini hali si hivyo....wanauza wachezaji tegemeo (makambo, nasikia tetesi fei toto yuko njiani pia) bila kureplace hii si dalili nzuri

    Mwisho wa Maoni...

    ReplyDelete
  4. Wewe ni nani unayechagulia watu timu ya kupenda?Eti si lazima apende Yanga!Who are you?Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake mradi havunji sheria.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic