Mkurugenzi wa Taasisi ya HIDECA
inayojihusisha na utunzaji wa mazingira ,Sara Pima (kushoto) akimkumbatia
mshindi wa tuzo ya mazingira, Upendo Mmari.
|
Wanawake nchini, jana Jumatano katika
kusherehekea siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) walidhihirishwa kuwa wako juu
wakati wakitoa tuzo mbalimbali za wanawake wanaofanya vizuri katika fani
mbalimbali ikiwemo mambo ya mazingira, afya, sheria, sayansi na teknolojia na
mambo mengine.
Hayo yaridhihirika kwenye kongamano la
thamani ya mwanamke na ajira binafsi lililoandaliwa na kampuni ya Purple Planet
chini ya Mkurugenzi Hilda Kisoka na kufanyika Ukumbi wa King Solomoni uliopo
Kinondoni, Namanga, Dar na kuhudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka mikoa
mbalimbali ya hapa nchini.
Joyce Likokola maarufu Mama Vicoba
akisindikizwa na wenzake kwenda kupokea cheti cha kutambua mchango wake kwenye
jamii.
|
Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa Mbunge
wa Hanang mkoni Manyara Dk. Mary Nagu ambaye alishuhudia ugawaji wa tuzo
mbalimbali kwa wanawake hao.
Miongoni mwa tuzo zilizotolewa kwenye
kongamano hilo ni tuzo ya afya ambapo wanawake waliojitolea maisha yao
kupigania afya za uzazi wa mpango, kupunguza maambukizi ya Ukimwi walitunukiwa
tuzo.
Wanawake wengine walioibuka na tuzo hizo ni
wanasheria waliowahi kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wenzao na watu
wengine wapotaka kupoteza haki zao kwa kukosa kipato.
Tuzo nyingine ilikuwa ni ya mazingira ambapo
wanawake kadhaa waliofanikisha zoezi la utunzaji wa mazingira na kutoa elimu
hiyo sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni sokoni na sehemu nyingine za
mikusanyiko nao walitunukiwa tuzo.
Wakulima nao hawakuachwa kwani wanawake
waliofanya vizuri kwenye sekta ya kilimo nao walitunukiwa tuzo.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wanawake
kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini.
Mgeni rasmi akimpa tuzo Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara mstaafu, Shamim Khan.
|
Kongamano hilo sambamba na kutawaliwa na
shangwe na nderemo kwa waliokuwa wakipokea tuzo na wapambe wao.
Pamoja na shangwe hizo mwanamuziki mkongwe
wa taarab, Patricia Hilary naye aliwanogesha wanawake hao kwa nyimbo zake
zilizowahi kutamba kama ule wa Njiwa Peleka Salamu, Jamani Mapenzi Yananitatiza
na Ni Mdodo.
Safi sana. Hongereni sana akina mama wa Tanzania. Serikali izidi kiwaamini na kuwawezesha na kuwashirikisha zidi akina mama katika harakati za maendeleo kwani ni njia pekee ya haraka kulifikisha Taifa kunako uchumi wa kati.
ReplyDelete