May 4, 2019


KESHO kikosi cha Simba kitamenyana na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine ikiwa ni mchezo wao wa 30 kwenye ligi.

Mpaka sasa Simba ambao ni mabingwa watetezi wamejikusanyia jumla ya pointi 75 wakiwa nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 80 akiwa amecheza michezo 34.

Wachezaji wawili ambao walikuwa majeruhi, nahodha, John Bocco na beki Pascal Wawa wanatarajiwa kuanza mazoezi na timu kesho huku Paul Bukaba akiwa nje ya mchezo kutokana na majeraha ya mguu aliyoyapata jana wakati wanamenyana na Mbeya City.

4 COMMENTS:

  1. Mechi ngumu kwa Simba na ni mechi ya fitna.Mechi ya kesho na prison haina tofauti na mechi ya Kagera sugar hasa ukichukulia maanani yakwamba Simba ikishinda hii mechi atakata pengo la points na Yanga na kumkaribia kabisa. Si ajabu kabisa prison kurudi Mbeya kutoka Dareslaam wakiambatana na watu wa Yanga kuja kuiwangia Simba kwa namna yeyote ile ili wapoteze mechi. Kama kuna mechi wachezaji na benchi la ufundi la Simba wanatakiwa kuondosha mzaha basi ni hii mechi ya kesho na prison.

    ReplyDelete
  2. Tunataka kikosi kamili Leo ishalla

    ReplyDelete
  3. Hakika tunataka kikosi kamili, prison ni timu bora sana kwa soka la Tanzania. Haitakiwi mzaha hapa

    ReplyDelete
  4. Tutawapiga wala mctie shaka wadau

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic