May 29, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji na mwekezaji wa timu hiyo, mfanyabiashara Mohammed Dewji wamekubaliana kwa pamoja kuipeleka timu hiyo nchini Marekani katika kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Aussems amekubaliana hivyo na Mo baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Na amefunguka hivyo katika mahojiano yake Jumatatu kwenye Hoteli ya Sea Scape jijini Dar jana.

Ikumbukwe kuwa huu ni msimu wa pili kwa timu hiyo kwenda kuweka kambi nje ya nchi baada ya mwanzoni mwa msimu huu kwenda Uturuki katika kambi ambayo imewapatia mafanikio makubwa.

Aussems alisema kuwa tayari wameshakubaliana na Mo kuwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao itafanyika katika nchi ya Marekani inayoongozwa na Rais Donald Trump.

“Maaandalizi ya msimu ujao tutaanza baada ya kukamilisha ligi ambayo Jumanne (kesho) ndiyo itakuwa inafikia mwisho baada ya kupewa kombe letu, kwa sababu tuna mengi ya kufanya ikiwemo suala la maandalizi ya kambi ya maandalizi kwa msimu ujao.

“Lakini tumeshakubaliana na jana nilikuwa na Mo mwenyewe kuongelea suala hilo wapi tutaweka kambi japokuwa uongozi wao walitaka zaidi twende tukaweke kambi nchini Ureno lakini nimemueleza Mo kwamba ni vyema tukaenda kuweka kambi nchini Marekani, jambo ambalo ameshalipitisha, hivyo kwangu nasubiria wakati uweze kufika,” alisema Aussems.

1 COMMENTS:

  1. Kutokana na mipango kama hiyo pamoja na Moo kuandikisha nyota wapya Kwa gharama kubwa sana Kwa mabilioni, bado Kuna viumbe wanatamka kuwa Simba yapendelewa haistahiki ubingwa. Hao ni mahassidi ambao Mungu anawalani na katu hawawezi kufanikiwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic