May 24, 2019


Mchezo wa Simba SC dhidi ya Biashara umerudishwa nyuma kwa saa moja kutoka saa 10 hadi saa 9 alasiri.

Sababu za maamuzi hayo ni sherehe za ubingwa zitakazoendana na kukabidhiwa kikombe cha Ligi Kuu Bara msimu huu.

Pia mechi hiyo iliyokuwa iepangwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru, sasa itafanyika katika Uwanja wa taifa.

SImba itakabidhiwa kikombe chake ambacho imetwaa msimu huu kwa mara ya pili mfululizo ikiwa ni baada ya kutwaa pia msimu uliopita.

5 COMMENTS:

  1. Ni haki ya Simba kukabidhiwa tu kombe hilo. Timu imejituma na imefanya kazi kubwa sana. Na imeonyesha ukomavu wa hali ya juu.

    Wachezaji hawakujali mbanano wa ratiba wala kusafiri na bila kupumzika mechi inachezwa. Maana katika hili iwapo wangekuwa wale wenzetu, wangelia sana kwa madai wanaminywa na ratiba na mambo mengine. Lakini sijawahi kusikia hata siku moja uongozi au wachezaji walalamikie jambo hilo. Pongezi sana kwao.

    ReplyDelete
  2. Ila kwa kupambana Simba wanastahili pongezi. Wanatolewa kwenye mechi za klabu Bingwa Afrika wana tofauti ya mechi 15 na huku wamecheza mfululizo na kupata matokeo kama hayo halafu wengine wanasema wamebebwa, jamani jamani Mungu anawaona.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Kwa miaka tele ijayo Simba atabakia bingwa wakitaka wasitake

    ReplyDelete
  4. Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna kiongozi wala mchezaji aliyelalamikia kucheza viporo vilivyokuwa na ratiba iliyobana bila mpangilio tena kinyume na kanuni za FIFA ya timu kucheza next match baada yaa masaa 72.Simba kuanzia viongozi, wachezaji,wanachama na mashabiki wamepambana na wanastahili mkono wa pongezi kwa kuchukua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ya Africa.Jirani mtatesekaa sanaa.

    ReplyDelete
  5. Zahera alisema haogopi hatosita kusema ukweli kuwa Simba haistahiki kuwa bingwa, basi hiyo kesho ni fursa Kwa Zahera kujitokeza na kuonesha msimamo wake usiotikisika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic