May 24, 2019

Liverpool, Manchester United na Arsenal wanataka kumsaini mchezaji nyota wa Colombia James Rodriguez, 27, ambaye anatarajiwa kuondoka Bayern Munich mkataba wake wa mkopo utakapokamilika msimu huu.
Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness amethibitisha kuwa mabingwa hao wa Bundesliga wanamtaka winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane.
City wanajiandaa kuweka dau la kumnunua nyota huyo wa miaka 23 kutoka kwa miamba hao wa ujerumani ambalo linatarajiwa kuvunja rekodi.
Arsenal wanataka kumsaini winga Ryan Fraser, 25, baada ya fainali ya ligi ya Europa, lakini Bournemouth wanataka kulipwa £30m kumwachilia kiungo huyo wa kimataifa wa Uskochi. (Independent)
Tottenham wamewasiliana na Real Madrid ili kuanza mazungumzo ya kutaka kumnunua kiungo wa kati Marco Asensio, 23, lakini wameambiwa mchezaji huyo rai wa Uhispania hapatikani. (AS - in Spanish)
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez amewambia Marseille na Roma kuwa kipaumbele chake ni kukubali mkataba mpya St James Park baada ya wao ku kuonesha ari ya kutaka kumpatia kazi ya umeneja.
Wachezaji Matteo Darmian, 29, Romelu Lukaku 26, Juan Mata, 31, na Marcos Rojo - huenda wakondoka Manchester United msimu huu.
Inter Milan itatangaza ofa ya zaidi ya Euro 30 m winga wa Croatia winger Ivan Perisic, 30, ili kumnunua Lukaku.
Manchester City wanataka Euro 15m kumuuza kiungo wa kati Fabian Delph, huku vilabu kadhaa vya ligi ya Premier vikimnyatia nyota huyo wa miaka 29. 
Mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke, 28, huenda akaondoka Selhurst Park msimu huu baada ya kukubali dau la euro 15 m la kumnuuza nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kutoka klabu ya China ya Shandong Luneng Taishan. 
Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic