KOCHA wa Ruvu Shooting, Ablumutik Haji amesema kuwa haamini macho yake kubaki ligi kuu kwani alikuwa anapitia kipindi kigumu msimu huu hali iliyomfanya akate tamaa.
Ruvu Shooting jana ilishinda mbele ya Alliance kwa bao 1-0 na kubaki kwenye ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 45 ikiwa nafasi ya 15.
"Ngumu kuamini ila mwisho wa siku namshukuru Mungu kwa kutupigania na kutupa nafasi nyingine msimu mwingine, tutapambana kwa hali na mali maana msimu huu haukuwa bora kwetu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment