May 29, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa T-Shirti lake alilokuwa analipenda kuvaa msimu huu halina bahati ya kubeba ubingwa hivyo msimu ujao atabadilisha ili abebe ubingwa.

Yanga jana wamepoteza mchezo wao wa mwisho mbele ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Zahera amesema kuwa sababu kubwa ya kuvaa T.Shirt hiyo ni nembo yake ambayo ameiteua msimu huu.

"Kila mmoja ana mtindo wake unaomtambulisha hivyo kwangu mimi T.shirt yangu ni utambulisho wangu pamoja na hii kofia, ila sasa nimeona haikuwa na bahati msimu ujao nitaboresha zaidi.

"Tumefungwa kwa kuwa wachezaji hawakuwa na morali kubwa ila hakukuwa na chochote cha kupoteza ila ni matokeo tu yametokea tumepoteza," amesema Zahera.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic