May 13, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa mbinu zake zote leo zilikwama mbele ya Azam FC hali iliyofanya aambulie suluhu.

Simba leo waliikaribisha Azam FC uwanja wa Uhuru mchezo ambao ulikuwa na ushindani kwa timu zote mbili na dakika 90 zimekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu kwa suluhu ya 0-0.

"Ulikuwa ni mchezo mzuri na mgumu, haikuwa hesabu zangu kupata pointi moja ila wachezaji walipambana na nilibadili mbinu zote kutafuta matokeo nimekwama.

"Nimefurahi namna ushindani ulivyokuwa na kila mmoja ameona namna wachezaji walivyojituma, nimefurahi kupata pointi moja," amesema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic