May 13, 2019


KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji wake wamebweteka baada ya kupata ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la FA uliochezwa uwanja wa Samora.

Matola amesema kuwa kupoteza kwao mbele ya Mbeya City kwa kufungwa mabao 3-0 kumetokana na kujisahau hivyo atakaa na wachezaji wake ili wabadilike.

"Baada ya kushinda mbele ya Yanga mabao 2-0, wachezaji wamejisahau na kubweteka, wanadhani wamemaliza kazi kumbe bado safari inaendelea.

"Nitakaa nao ili kuwaambia kwamba waache kubweteka kwani kuifunga Yanga haimaanishi tumemaliza ligi, bado tuna kazi kubwa ya kufanya na kupambana ili kupata matokeo chanya," amesema Matola.

1 COMMENTS:

  1. Goli 4zinawasubiri,mbinu zote zinaishiia kwa yanga,refa,uwanjawa nyumba mwisho wa siku mnacharazwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic