May 2, 2019


MGOMBEA wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Yanga, Magege Chotta ameweka wazi kuwa iwapo atapata nafasi ya kuchaguliwa ndani ya klabu hiyo kongwe atawaleta wawekezaji wa maana.

Chotta ni miongoni mwa wagombea 29 wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Klabu ya Yanga katika uchaguzi unaofanyika Jumapili hii, jijini Dar es Salaam.

Chotta alisema kuwa, kuna wadhamini wengi ambao
wamelenga kuwekeza ndani ya klabu hiyo ambapo wanasubiria viongozi wapya waingie madarakani ndipo wajitokeze.

“Kuna wawekezaji wakubwa wapo mbioni kuja kuwekeza Yanga na mimi nalijua hilo, tayari nimeshazungumza na watatu ambao wamekubali kuja Yanga, ni watu wenye fedha zao, wanajiweza, walikuwa wanasubiria uchaguzi ufanyike tu ndiyo waje.

“Wengi wao walikuwa wakihitaji kuwekeza lakini ilishindikana na kuhofia kutoa fedha zao sehemu ambayo hakuna uongozi hivyo waliofia kupoteza.

“Uchaguzi huu ukifanyika kila kitu kitakwenda sawa na Yanga inakwenda kuwa moja ya klabu yenye mafanikio makubwa hapa nchini hivyo naomba wanachama wanichague ili niweze kufanyia kazi mabadiliko hayo,” alisema Chotta.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic