May 13, 2019


KOCHA wa timu ya Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa leo Simba walikuwa wana bahati kwani walijipanga kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 mzunguko wa kwanza mvua imetibua mipango.

Azam FC leo wamegawana pointi moja na Simba uwanja wa Uhuru baada ya kushindwa kupata matokeo ndani ya dakika 90 baada ya kutoka na suluhu ya bila kufungana.

"Tulijipanga na tulidhamiria kushinda leo, hizo ndiyo zilikuwa hesabu zetu bahati mbaya mvua imetibua mipango yetu hali iliyofanya tugawane pointi moja.

"Tunaitambua Simba vizuri kutokana na uzoefu, kwa sasa tunaachana na mchezo wa leo hesabu zetu ni kulelekea michezo iliyobaki kwenye ligi," amesema Cheche.

Ushindi wa leo unaifanya Azam FC ijikite nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 36 ikiwa nafasi ya tatu imebakiwa na michezo miwili mkononi baada ya kucheza michezo 36 na ina pointi 69.

3 COMMENTS:

  1. AMA KWELI HIVI MCHEZO WA LEO WALIOKOSWAKOSWA NI NANI SIO AZAM? WENYE BAHATI LEO NI AZAM KUTOFUNGWA WALICHEZEWA SANA HASA KIPINDI CHA PILI

    ReplyDelete
  2. Huyu kocha kasema wamekaa nyuma ili simba wasiwafunge baadae simba wanabahati mvua imewaokoa uhalisia wamechezewa nusu uwanja too contradiction!upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  3. Hii timu nayo ianataka kufanana na waleeee jamaa zetu, kila mtu msemaji matokeo yake wanakinzana kauli.

    Kocha mkuu Kasema walipaki basi ili wasifungwe na Simba (Maana yake walihofia kufungwa na Simba / Hawajiamini / Wanaiogopa Simba).

    Kocha msaidizi (Cheche) anasema kuwa malengo yao yalikuwa ni kuifunga Simba! Jamani, au Kocha mkuu anapanga na wachezaji kivyake malengo ya mechi na pia naye Msaidizi anajifungia na wakwake kivyake na kila mmoja anaweka malengo yake?!.

    Kingine cha kuchekesha, aliyetekwa anatamba kuwa naye alimteka mtekaji!!! Si kichekesho hiki.

    Bila ushabiki, Jana Azam mmeponea kwenye ncha ya Kisu. Mnapaswa Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa matokeo yaliyotokea. Imani yangu ni kuwa yale matokeo ninyi Azam ndiyo ambayo mliyatarajia na kujipanga nayo.

    Ni ngumu timu inayotafuta ushindi, dakika ya 32 Golikipa anaanza kupoteza muda. Dakika za 60 ..... 70...... mabeki na mawinga wanajivuta kwenda kurusha mipira iliyotoka!, Wachezaji wanajiangusha bila kuchezewa faulo na kuonyesha wameumia! Maana hata Dakika 4 zilizoongezwa zinaonyesha kuna timu ambayo imepoteza muda bia sababu, na ndio maana mpira ukaenda hadi dakika 96.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic