May 24, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema Simba wamepata faida kubwa sana ya kucheza na klabu kubwa kama Sevilla.

Taarifa imesema kuwa Zahera amefunguka kuwa ingawa Simba walifungwa ila walicheza mpira mzuri hasa kipindi cha kwanza.

Zahera ambaye ni raia wa Congo amewaomba wadhamini wao Sportpesa ambao ndiyo waliileta Sevilla Tanzania msimu ujao na wao wacheze na timu kubwa kama walivyocheza Simba ili kuwapa uzoefu wachezaji wake.

SImba ilicheza mchezo huo jana katika Uwanja wa Taifa na kufungwa idadi ya mabao 5-4 na ukiweka historia kwa timu bingwa mara tano katika UEFA Europa League.


4 COMMENTS:

  1. Wewe subiri sevilla ya kutoka rufiji, maana huna jema kila kitu kwako kibaya. Unaonewa tu

    ReplyDelete
  2. Kaa ukiingoja lakini hamutowaona kwasababu Hamna sifa na pindi mukiipata fursa basi mtaadhirika

    ReplyDelete
  3. naona wazee wa kujisifu mpira mwingi hamsa palepale

    ReplyDelete
  4. Mnafungwa na Lipuli halafu Una diriki ku comment .Kweli uso wa mbuzi hauoni aibu.Vipi ligi imekwisha?Waingereza wanaiita house warming. Yaani ukae kwenye nyumba ya wenyewe mpaka wenyewe warudi halafu uende kupanga.Poleni vyura kwa kutulindia kikombe chetu.Mlikuwa mawatch men wazuri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic