ALIKIBA AUNGANA NA CHUMA ' MEDDIE KAGERE' KUMMALIZA SAMATTA LEO, TAZAMA TIZI LAO - VIDEO
Msimu mpya wa 'Nifuate' ya msanii, Alikiba na mwanasoka, Mbwana Samatta imekuja kivingine huku wakitambiana kuelekea mchezo wao wa hisani, Juni 2 utakaochezwa Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Viingilio katika mchezo huo ni Sh.2000 kwa viti vya mzunguko, eneo maalumu yani vip B ni Sh.2000 huku maalumu zaidi 'Champion' ikiwa Sh. 5000.
Nifuate ni kampeni maalumu imeanzishwa na mastaa hao kupitia taasisi yao ya Samakiba yenye lengo la kuungana na wadau wengine ili kwa pamoja waiguse jamii kwenye maeneo mbalimbali.
Katika uzinduzi wa kampeni hizo, Samatta alisema watatumia mchezo huo kama ilivyokuwa msimu uliopita kuchangisha kipatikanacho ili kwa pamoja warudishe kwa jamii.
"Nianze kwa kusema shukrani kwa Watanzania wote ambao wamelipokea hili vizuri tangu msimu wa kwanza hadi hivi sasa ambapo wengi wanaonekana kuguswa nalo.
"Lengo letu ni kuirudishia jamii na safari hii tutajikita wenye mambo matatu, ambayo ni kutoa misaada kwa yatima, kusaidia walemavu na kusaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu," alisema Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment