NYOTA wa
timu ya Simba, Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anazidi kuwa mtamu kwenye michuano
ya Afcon inayoendelea nchini Misri amewavuruga mabosi wa Simba baada ya
kutoweka wazi hatma yake ya kurejea Simba.
Okwi mpaka
sasa kwenye michezo miwili ya Afcon ambayo Uganda wamecheza dhidi ya Congo
pamoja na Zimbabwe amefunga mabao mawili na kuibuka mchezaji bora kwenye mchezo
mmoja dhidi ya Congo hali inayomuongezea thamani.
Okwi amesema
kuwa anajivunia kuwa na mashabiki wa Tanzania hali inayompa furaha hivyo wakati
ukifika kila kitu kitakuwa sawa kwake kutaja hatma yake na Simba.
“Nafurahi
kuwa na mashabiki wengi kutoka Tanzania nawapenda, kuhusu kurejea Simba kwa
sasa ni ngumu kulizungumzia ila wakati ukifika itafahamika tu,” amesema Okwi.
Mtendaji
Mkuu wa Simba Crescetius Magori amesema kuwa kwa sasa wanafanya mazungumzo na
wachezaji waliomaliza mkataba endapo watafikia makubaliano watawasainisha ili
kuendelea kupata huduma zao.
0 COMMENTS:
Post a Comment