LICHA ya
timu yake kushindwa kufurukuta kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini
Misri, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma kurudi mapema Bongo endapo
atapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zimbabwe.
Zahera kwa
sasa yupo na kwenye benchi la ufundi la timu ya Congo akiwa ni kocha msaidizi na timu yake ipo mkiani kwenye kundi A baada ya kupoteza michezo
yote miwili kwa kufungwa na Uganda pamoja na Misri.
Zahera
amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurejea Tanzania kuanza kukikonoa kikosi chake
cha Yanga badala yake atakwenda Ufarasa kula bata na familia.
“Nimkekaa
muda mrefu Tanzania nikiwa na timu yangu ya Yanga, kwa sasa sifikirii kurejea
mapema kuanza maandalizi kwani ni muda wangu wa kupumzika na mke wangu.
“Mchezo wangu wa mwisho utakuwa tarehe 30 nina
imani ya kufanya vizuri kwani tayari kwa sasa wachezaji wamepata uzoefu na nina
imani ya kushinda kama tukipoteza basi nitakwenda zangu Ufarasa kupumzika na
familia,” amesema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment