June 15, 2019

RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amesema viongozi wa Serikali hawatakiwi kuegemea katika klabu moja na kukandamiza nyingine kwa sababu zote ni za Watanzania na wao ni viongozi wa Tanzania.

Kikwete amesema kuwa yeye akiwa Rais aliwahi kuwapa Simba pesa kiasi cha sh milioni 30 kwa ajili ya kununua eneo la Simba.

Kikwete amesema wakati akitoa neno kwenye hafla ya uzinduzi wa harambee ya kuichangia Yanga katika Ukumbi wa Diamond jubilee, jijini Dar es Salaam.

“Kuna wakati Prof. Sarungi na Juma Kapuya walikuwa Mawaziri wa michezo na hawa wote ni Simba kindakindaki lakini hawakutumia nafasi zao kuikandamiza Yanga. 

"Nilipokuwa Rais Simba walitaka kununua kiwanja kule Mabwepande lakini hela hawana, Aden Rage alikuja kwangu kuniambia wanahitaji milioni 30 kwa ajili ya Kiwanja nikawaambia hizo mmepata.

“Nayasema haya kwa uwajibu wa Uongozi. kwahiyo Mhe. Waziri Mkuu, Yanga wana shughuli na wewe utoe sikukumbushia kama deni ila nawaombea Wanayanga wenzangu mchango ukamuambie na Mhe. Rais na yeye atoe," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Amenena vyema Mheshimiwa rais mstaafu.Kuna watu wawili wanatumia nafasi zao vibaya kuikandamiza Yanga kwa namna wanavyotaka wao na hili nina hakika mheshimiwa Kikwete analijua na ndio maana kaamua kufunguka ili wasikie na waache.Wasidhani wana uwezo wa kuburuza watu jinsi watakavyo katika nyanja zingine na hayo yakavumiliwa kwenye sekta ambazo zinakutanisha watu wenye itikadi tofauti tena zenye nguvu kama michezo au dini.UJUMBE UMEWAFIKIA

    ReplyDelete
  2. Kazingua huyo kutoa ni moyo sio figo aaah sio lazma

    ReplyDelete
  3. tatizo la waandishi wetu wa michezo ni vilaza wao kazi yao ni kuandika hivi hakuna hata mwandishi mmoja mwenye kumbukumbu ya harambee waliyofanya timu ya simba kipindi cha uongozi wa rage pale alipowaeleza wanachama zinatakiwa milioni 30 kwa ajili ya uwanja nilitegemea baada ya kauli ya rais mstaafu wangetoka waandishi wa habari na kwenda kumhoji Aden Rage zile pesa alizowachangisha wana simba wamepeleka wapi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic