June 18, 2019


BAADA ya Yanga juzi Jumamosi kutikisha katika usajili kwa kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda, Juma Balinya ambaye alikuwa akitakiwa na Simba sasa siri ya usajili huo imefichuka.

Wakala wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, Patick Gakumba, ambaye alipewa jukumu la kuhakikisha Balinya anatua Simba na uongozi wa timu hiyo amefunguka kila kitu kuhusiana na kilichotokea kwa mshambuliaji huyo ambaye amemaliza Ligi Kuu ya Uganda akiwa amefunga mabao 19 na kutua Yanga.

Gakumba alisema kuwa sababu kubwa ya Balinya kutua Yanga ni kutokana na uongozi wa Simba kushindwa kufikia makubaliano juu ya usajili ya mchezaji huyo.

“Kilichotokea ni vongozi wa Simba wao kwa wao kushindwa kukubaliana juu ya uwezo wa mchezaji huyo, baadhi walikuwa wakitaka asajiliwe lakini wengine wakigoma.

“Waliokuwa wakigoma walidai kuwa hana rekodi nzuri katika michuano ya kimataifa japokuwa ana rekodi nzuri ya ndani ya nchi yake na wao wanataka mchezaji mwenye rekodi nzuri ya kimataifa kwa ajili michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo timu hiyo itashiriki baadaye mwaka huu.

“Kwa hiyo, kutokana na hali hiyo viongozi hao waliamua kuachana naye japokuwa kila kitu kuhusiana na usajili wake kilikuwa kimekamilika na kilichokuwa kimebakia ni yeye kuja kusaini tu.

“Hali hiyo ndiyo iliyomfanya meneja wake akachukua uamuzi wa kuzungumza na Yanga nao bila kuchelewa wakaamua kumsajili, ila kusema kweli Simba wameacha bonge la mchezaji,” alisema Gakumba.

7 COMMENTS:

  1. Bonge la mchezaji hata kikosi cha akiba cha the crane hayumo?

    ReplyDelete
  2. Mbona hata Mkude, Kakolanya, Kotei, Salamba na Dida hawapo timu za Taifa?

    ReplyDelete
  3. Kwnn wasimsajili Salum Aiyee, mbona analingana magoli na huyo Balinya??? Au ndio ile kutokuthamini cha kwetu???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisa huyu ni sawa na ayee tu maana hata timu yake ipo ya 11 kati ya Tim 16

      Delete
  4. KOTEI NI MCHEZAJI WA NDANI !!!! MBONA MNATETEA BILA KUFIKIRI !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kotei alitokea kwenye ndondo cup ya kwao Ghana

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic