June 30, 2019



DANNY Lyanga amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kujiunga na kikosi cha JKT Tanzania baada ya kuachwa na Azam FC na kukamilisha jumla ya wachezaji sita waliopigwa pini na JKT Tanzania.


Lyanga ameungana na wachezaji wengine watano waliosajiliwa na JKT Tanzania ambao ni pamoja na Jabiri Aziz ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja akitokea African Lyon, Hafidhi Mussa ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ametokea Stand United.

Mshambuliaji Adam Adam kutoka Tanzania Prisons amesaini kandarasi ya mwaka mmoja, Adeyum Saleh kutoka Coastal Union amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na Hassan Mwaterema amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic