June 22, 2019


KIPA Juma Kaseja ‘Tanzania One’ ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu yake ya KMC aliyoichezea msimu uliopita.

Kaseja amesaini mkataba huo leo Jumamosi huku ukiwa ni mwendelezo wa timu hiyo kubakiza nyota wake ambao waliokuwa nao msimu uliopita.

Akiwa na kikosi hiko Kaseja amewapa changamoto makipa wenzake, Jonathan Nahimana pamoja na Dennis Richard hali iliyofanya kikosi hicho kuwa imara.

Kipa huyo ameiongoza KMC akiwa Nahodha ambapo walimaliza ligi wakishika nafasi ya nne kutokana na mwenendo mzuri ikiwa chini ya kocha Ettien Ndayiragije ambaye sasa ni kocha wa Azam FC.

Wachezaji wengine walioongezwa mikataba ni Charles Ilanfya, Dennis Richard, Rehan Kibingu, Sadala Lipangile, Cliff Buyoya, Ismail Gambo, Omary Ramadhan, Abdul Hillary, Ally Ramadhan na Rayman Mgungila.

KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni itashiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, ikiwa ni mara yao ya kwanza tangu ipande Ligi Kuu ambayo pia wamecheza msimu mmoja pekee.

1 COMMENTS:

  1. Kwangu mie Juma Kaseja namuhesabu hadi sasa kama golikipa No.1 Tanzania.Wanadai umri wa Kaseja ni mkubwa lkn angalia magolikipa maarufu hapa duniani na walioko Afcon kina Denis Onyango wana miaka mingapi? Mara nyingi golikipa na defenders wakiwa na umri mkubwa ndio wanakuwa na Exprience zaidi...chukulia mfano wa Kelvin Yondani,Aggrey Moris au Kompany ni mabeki ambao wamekomaa na uzoefu.
    Ningekuwa kwenye benchi la ufundi la Simba au Yanga ningemsajili Kaseja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic