MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeremiah amesema kuwa kwa sasa anapambana kujitoa kwenye dhambi moja ya kuzini kwa kujipatia jiko lake hivi karibuni.
Kala Jeremiah kwenye ngoma yake ya 'Dear God' ambayo ilimtambulisha vema alisema kwamba "Nisamehe dhambi ya kuzini" hali iliyomfanya ajithmini.
"Kwa sasa nipo kwenye mpango wa kuoa ili niepukane na dhambi niliyoomba msamaha, pia nashukuru mashabiki kwa sapoti wanayonipa kwenye kazi zangu wazipokee pia kazi zangu ambazo naendelea kuzitoa kama ambavyo nimefanya kwa sasa ambazo ni pamoja na Nisamehe na America," amesema Kala.
0 COMMENTS:
Post a Comment